Franco alisema kuwa ni salama kuimba kwa lugha ya Lingala. Hakuna ubaya kuongea kwa lugha yako. Kupitia Francois Luambo Luanzo Makiadi (Franco), lugha ya Lingala inajulikana katika Afrika na dunia yote.
Bila kuwa na aibu ya lugha yake, Franco na kundi lake la TP OK Jazz walitumbuiza mashabiki wengi duniani na kuwa mmoja wa wanamuziki tajiri katika Afrika. Imesemekana kuwa Franco alikuwa mfalme wa gitaa katika Afrika.
Franco aliimba na kutoa nyimbo zaidi ya 150. Hakuna mwanamuziki yeyote katika bara la Afrika ambaye ameweza kuvunja rekodi hiyo mpaka leo. Baadhi ya nyimbo zake nzuri zinafuata. Simba wa muziki katika Afrika. Ahsante Franco kwa kazi nzuri. Burudika.

Comments